UONGOZI wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), leo umefanya ziara Wizara ya Fedha na Mipango na kufanya mazungumzo na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Philip Mpango, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo wa Shirika la Posta uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanal Mstaafu Dkt. Harun Kondo, akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Deogratius Kwiyukwa,Kaimu Meneja Mkuu wa Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bw. Elia Madulesi.

Katika mazungumzo hayo, ujumbe kutoka Shirika la Posta ulimweleza Waziri hali halisi ya Shirika, zikiwemo changamoto , mafanikio na maendeleo ambayo shirika limeyapata tangu lilipoanzishwa mwaka 1994 baada ya kutenganishwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Benki ya Posta ambao kwa sasa ni taasisi zinazojitegemea kama ilivyo Shirika la Posta.

Mwenyekiti alieleza juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Shirika katika kulifanyia mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiutendaji ili liweze kukabiliana na changomoto za ushindani wa huduma na biashara kwa jumla.Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Harun Kondo, alimwomba Waziri Mpango, alisaidie Shirika katika kutatua changamoto mbali mbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa na kulia ni Mkurgenzi wa Sera wa wizara hiyo, Bw. Mgonya Benedicto.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa.

Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini, mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mchumi Mkuu wa wizara, Dionisia Mjema.(Picha zote na Bw. Elia Madulesi).

Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Posta wakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango(wa pili kushoto) baada ya ujumbe huo kumtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...