Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao (katikati)
na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakionyesha mabango yanayoelekeza
jinsi yakupata vifurushi vya bando la”Pinduapindua” kwa ajili ya wateja
wao hususani vijana wakati wa uzinduzi wa bando hilo ambapo mteja
anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha
wiki au cha mwezi,Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano, Jaquiline Materu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Nandi
Mwiyombela ,Mkurugenzi wa Masoko, Hisham Hendi na Mkuu wa Kitengo
cha Bidhaa na Huduma kwa Wateja, Linda Riwa.
Vijana wakitanzania na wateja wote kwa ujumla wa Vodacom Tanzania
PLC,wameletewa Uhuru na wepesi zaidi wa kutumia bando jipya
la”Pinduapindua” lililozinduliwa jana na kampuni hiyo likiwa mahususi
kwaajili ya wateja wa mtandao huo.
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo,Mkurugenzi wa biashara
na Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Hisham Hendi alisema
huduma ya bando hili jipya la “Pinduapindua” ni ya kwanza na
yakihistoria katika kampuni zote za mawasiliano nchini,Hii ni moja ya
mikakati ya kampuni yetu kutaka kuleta mabadiliko kwenye jamii
hususani vijana kwa kuwarahisishia maisha yao ikiwemo kuongeza
vipato na dhamira kubwa yakuwapeleka watanzania katika ulimwengu
wa sayansi na teknolojia.
“Utafiti wetu unaonyesha kwamba vijana ni moja ya kiungo kikubwa sana
kwa mapinduzi yakiuchumi nchini pia ni tabaka linalokuwa kwa kasi ya
kuridhisha na wana mahitaji maalum yakipekee yakiteknolojia tunapenda
vijana watambue kwamba Vodacom Tanzania PLC imesikia kilio chao
ndiyo maana leo hii tumewaletea Pinduapindua ”, alisema Hendi.
Pinduapindua ni kifurushi huru na chakipekee zaidi kuliko vifurushi
vingine vinavyowapangia wateja wa kampuni zingine za mawasiliano
nchini,Bando hili litawapatia vijana na wateja uhuru wao wa kuchagua
kiasi cha kupangia kwenye data, kupiga simu (voice) au ujumbe mfupi
(SMS) kulingana na mahitaji ya wakati huo. “Pinduapindua” pia
itamwezesha mteja kutumia Facebook (ikiwa pamoja na picha),
Whatsapp (maandishi na picha) na SMS hadi 200 bure.
Mkurugenzi huyo alifafanua zaidi kwamba kampuni inaelewa kwamba
mahitaji ya wateja wao ya utumiaji hubadilika siku hadi siku kuna siku
unaweza kuhitaji matumizi ya mtandao (data) zaidi ya muda wa
maongezi, kwa hiyo unakuwa huru kupangilia matumizi ya kifurushi
chako kuendana na mahitaji yako na jinsi yakupata vifurushi vya bando
hili ni rahisi mteja atahitaji kupiga namba *149*01# kisha kuchagua
kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi. Vifurushi hivi vinaweza
kulipiwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa na mara baada ya
kununua, mteja atapatiwa kifurushi chake, Facebook BURE, Whatsapp
BURE na SMS, vyote ambavyo vitatumika kwa muda wote wa kifurushi
alichochagua” alisema Hendi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao (katikati) akicheza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa bando jipya la Pinduapindua kwa ajili ya wateja haswa vijana,Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili mteja anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi.
Wacheza shoo wa promosheni ya bando la Pinduapindua la Kampuni ya Vodacom Tanzania wakicheza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam jana. Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili mteja anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...