WAFANYABIASHARA katika Soko la Ilala Mchikichini wamepatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia masokoni .
Katika hatua nyingine wafanyabiashara wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wanawake wametakiwa kwenda kushitaki ofisi za masoko husika ili sheria ichukue mkondo wake kwa wahusika waweze kujirekebisha.
Mwito huo umetolewa na Mwezeshaji wa Sheria masokoni, Khadija Mohamed kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG) wakati wanasheria wa shirika hilo wakitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo hii.
"Wakina baba mnapofanyiwa vitendo vya kijinsia na wanawake katika masoko msione haya nendeni kushitaki kwa viongozi wa masoko ili watuhumiwa waweze kukamatwa na kujirekebisha" alisema Mohamed.
Mohamed alisema vitendo vya ukatili wa jinsia hawafanyiwi wanawake pekee bali hata wanaume wamekuwa wakifanyiwa lakini wanaona aibu kwenda kushitaki.Mwezeshaji wa Sheria Batuli Mkumbukwa alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo vimeshamiri hivyo alitoa mwito kwa wafanyabiashara wa soko hilo kuviacha.
Mwezeshaji wa kisheria kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Amina Mussa akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo.
Mfanyabiashara Shikei Ngosi, akielezea changamoto zinazotokana na ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mwezeshaji Khadija Mohamed akitoa elimu ya upingaji wa ukatili wa kijinsia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...