MTANDAO
wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na
Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora
inapatikana nchini Tanzania.
Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.
Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.
Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.
Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.
Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.
Sehemu
ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika
kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...