Mkurugenzi
wa shule ya Feza Ibrahim Yunus kushoto na kulia Mwalimu Mkuu wa Feza Boys,
Saimon Albert wakiwa kwenye picha ya
pamoja na mshindi wa kwanza hadi watatu wa mashindano hayo. Wa kwanza kushoto
ndiye Perfect Ndyetabura aliyeibuka
mshindi wa kwanza kutoka shule ya msingi Hazina na Hamza Azaeli mwenye miwani aliyeibuka
mshindi wa pili naye akitokea shule ya Hazina na watatu anatoka shule ya Feza.
WANAFUNZI wa
shule ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi kwenye
mashindano ya Genius CUP, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi aliyeshika
nafasi ya kwanza kwenye mashindano hayo
ni Hamza Azaeli na Perfect Ndyetabura ambao wote wanatoka shule ya msingi
Hazina.
Mashindano
hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali nchini yaliandaliwa na shule ya Feza na kushirikisha shule kutoka
mikoa na kuitaja baadhi ya mikoa iliyoshiriki kuwa ni Tanga, Mwanza, Dodoma,
Mbeya, Mtwara, Pwani, Arusha na Zanzibar.
Mratibu wa mashindano hayo kutoka
shule ya Feza, Ashrak Habibu, alisema wanafunzi hao walionyeshana umwamba
kwenye masomo ya sayansi na hisabati.
Katika hafla ya kukabidhi vyeti hivyo,
iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Kimataifa ya Feza, Salasala jijini Dares Sallam,
Mkurugenzi wa shule hiyo, Ibrahim Yunus alisema mashindano hayo ya kimasomo
yajulikanayo kama Genius Cup, yaliandaliwa kwa pamoja na shule hizo kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Sayansi na
Teknolojia.
“Lengo letu ni kuwaandaa wanafunzi ili
watakapomaliza masomo yao wawe na taaluma ya kisayansi, hasa kwa kuwa nchi
inaelekea katika uchumi wa viwanda, hivyo inahitaji vijana wanasayansi na
mashindano haya hufanyika kila mwaka hapa nchini,” alisema mkurugenzi huyo.
Mbali na kupewa vyeti, wanafunzi watatu
waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya Hisabati walitunukiwa kiasi cha fedha
200,000 kwa mshindi wa kwanza (150,000) mshindi wa pili na laki moja kwa
mshindi wa tatu.
Akizungumzia
mafanikio ya wanafunzi hao, Mwalimu Mkuu
wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema wanafunzi
wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vyema kwenye mashindano mbalimbali kutokana na
maandalizi mazuri wanayoyapata.
“Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa
wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule
unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia wanafunzi wetu
kufanya vizuri kwenye mashindao mengi,” alisema Mwalimu Patrick
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...