Wahamiaji Haramu wakisubiri kusomewa mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali leo jijini Dar es Salaam Katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wahamiaji 40 kutoka Ethiopia wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam leo na kukutwa na mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.
Wahamiaji haramu wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuwasiri tukoka walipokuwa wamehifadhiwa.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Karama Kenyunko,
Blogu ya jamii.
WATANZANIA wawili, Ibrahim
Abdallah dereva wa gari aina ya Nissan Civilian namba T 669 DJH na
kondakta Christopher Steven wamepandishwa katika kizimba cha mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha binadamu kimagendo
ambao raia 31 wa Ethiopia.
Aidha raia hao 31 wa Ethiopia
wamesomewa mashtaka matano ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na
kibali.
Mwendesha mashtaka
wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Novatus Mlay amedai Septemba 25, mwaka huu, huko
Tuangoma wilaya ya Temeke watanzania hao walikutwa wakiwasafirisha raia
hao 31 wa Ethiopia kimagendo na kuwaingiza nchini kwa nia ya kuwapitisha
na kuwasaidia kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini.
Hata hivyo, watanzania
hao wamekana kuhusika na kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11,
mwaka huu huku upande wa mashtaka ukieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika
huku watuhumia hao 31 wa Ethiopia wakikubali mashtaka yote waliyosomewa na kesi
iendelea Oktoba 11, 2017 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Wakati huo huo, watanzania watatu
akiwamo dereva wa kampuni ya Dangote Cement Ltd, Khalid Abdallah, Hussein
Hamad Hassan na Jumanne Mtambo pamoja na wahamiaji nane raia wa Ethiopia
wamesomewa mashtaka matano likiwemo shtaka la kusafirisha kimagendo binadamu
na kuingia nchini kinyume cha sheria.
Wakili Mlay amedai
mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kuwa, wahamiaji Solomon Ertiso, Gazahegn
Tiroro , Haire Latso, Thadius Lilanso, Dawit Habtam, Deznet Godebo,
Feraru Gurana na Elioj Akola, Septemba 20,2017 katika eneo la Kongowe Mbagala
walikamatwa wakiingia nchini bila ya kuwa na kibali.
baada ya kusomewa mashtaka
hayo washtakiwa hao wote walikubali kuyatenda makosa hayo huku
watanzania hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu wanao
wanadaiwa kuwasafirisha kimagendo wahamiaji hao haramu.
Mlay alidai kuwa siku
hiyo ya tukio ya Septemba 20, 2017 huko Mbagala Kongowe Khalid,
Hussein na Jumanne wakiwa raia wa Tanzania walikutwa
wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu kimagendo.
Alidai kuwa raia hao
watatu wa Tanzania waliwasafirisha kimagendo wahamiaji hao haramu
kwa kutumia gari yenye namba za usajili T 961 DKA mali ya kampuni ya Dangote
Cement Ltd kwa kuwatoa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini.
Pia washtakiwa hao,
kuwa siku hiyo walikutwa wakisaidia kuwasafirisha wahamiaji hao ambao ni raia
wa Ethiopia kimagendo kwa kuwaingiza ndani ya jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Watanzania hao wamekana
tuhuma hizo na kesi hiyo itaendelea Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa huku Octoba
11 Raia hao wa Ethiopia watasomewa maelezo awali baada ya kukubali kutenda
makosa hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...