Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabati cha Kampuni ya ALAF Kanda ya Dodoma, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (mwenye tai), Waheshimiwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Viwanda pamoja na Viongozi wajuu wa Kampuni ya ALAF Tanzania wakishirikiana kukata utepe pamoja na kuashilia ufunguzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF kanda ya kati mjini Dodoma.
Kampuni ya ALAF (Tanzania) imefungua tawi lake jipya Mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma kwa wananchi baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema "Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali yetu inafanya kila linalowezekana
kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuwekeza kwa
kulinda mitaji yao kupitia kuondoa ushindani usiokuwa wa haki hasa unaotokana
na baadhi ya wafanya biashara kudanganya thamani ya bidhaa za bati
zinazoingizwa toka nje ya nchi na kulipa kodi pungufu, kudhibiti uingizaji
wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zaidi kulinda amani na maelewano
yaliyopo baina ya Serikali na wadau mbalimbali ili kujenga ustawi wa nchi yetu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua jiwe la msingi la kiwanda cha mabati cha ALAF Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa mikoa ya kanda ya kati (Dodoma, Singida na Tabora), Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Waziri Mwijage aliendelea kwa kusema “Napenda kuwashukuru
Kampuni ya ALAF (Tanzania) Ltd kwa kutekeleza vizuri maelekezo ya Sera ya
Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma zao kwa wananchi wa Dodoma baada
ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty alisema "uwekezaji
huu wa Dodoma ni wa thamani ya shilingi bilioni tatu ukiajiri watu 15 moja kwa moja
na wengine zaidi ya 100 ajira zisizo za moja kwa moja kama kupakia na
kushusha bati, kusafilisha bati, huduma za maji, stationary n.k."
Pia aliongeza kwa
kusema "ALAF inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo uagizaji wa
bidhaa sizizokidhi viwango unaofanywa na makampuni mbalimbali na pia
ukwepaji wa kodi, kupelekea serikali kukosa mapato stahiki na walaji kutumia
bidhaa zilizo chini ya viwango na hii hupelekea kukatisha tama wawekezaji wa
ndani ambao wanajitaidi kuzalisha bidhaa zenye ubora na kulipa kodi zote
stahiki.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akimueleza jambo Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
ALAF imekuwa ikishiliki
kwenye kama vile elimu, makazi, afya na mazingira.Mpaka sasa ALAF imetumia takriban shilingi milioni 200 kwenye mradi wa kuwaelimisha wafanyakazi na jamii kuhusu
ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa kushilikia na shirika la fedha duniani.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...