Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda jana amefunga rasmi zoezi la Siku
tano la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi wa Dar es salaam, ambapo
amewasihi Wananchi kujiwekea utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara.
Hadi kufikia majira ya Mchana zaidi ya Wananchi 11,000 walikuwa tayari wamepimwa afya zao,Makonda amesema lengo ni kuhakikisha Wananchi wote zaidi ya 20,000 waliohudhuria wanapimwa na watakaobainika kuwa na matatizo ya kiafya Wanapatiwa Matibabu.
Makonda amewashukuru Madaktari,Wauguzi,Askari Polisi, Vyombo vya Habari,Watu wa Usafi na Wadau wote waliojitoa kumuunga mkono hadi kufanikisha zoezi hilo.
Amesema kuwa Zoezi hilo la Siku tano limefanikiwa kwa 100% huku likigharimu kiasi cha zaidi ya Shilling Billion Moja ikihusisha Vipimo,Matibabu,Vyakula, Vinywaji ambapo gharama zote hizo zimegharamiwa na Wadau wa Maendeleo waliojitolea kumuunga mkono RC Makonda
Aidha RC Makonda amewapongeza Wananchi wote waliojitokeza na kuchangia Damu kwakuwa kiasi cha Damu walizochangia zitakwenda kuokoa maisha ya Wagonjwa.
Upimaji wa Afya ulihusisha Magonjwa yote ikiwemo Saratani, Kisukari, Presha, Macho, Homa ya Ini na Ugonjwa wa Moyo ikihusisha Madaktari bingwa na Wauguzi zaidi ya 300 kutoka Hospital za Umma, Jeshi na za Watu Binafsi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda akizungumza na wananichi katika wiwanja vya mnazi mmoja,wakati akifunga rasmi shughuli za upimaji Afya lililofanyika kwa siku tano ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar
Upimaji wa Afya kwa wananchi ukiendelea kufanyika ikiwa ni siku ya mwisho
Rc Makonda akisalimiana na mmoja wa watoto katika viwanja vya Mnazi mmoja,wakati wa shughuli za upimaji Afya kwa wananchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...