Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa madiwani kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepuka kuisababishia serikali hasara.
Jaji Kaijage ameyasema hayo leo (Tarehe 15.10.2017) mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.“…Tusipozingatia na kufuata taratibu za uchaguzi tunaweza kusababisha kesi nyingi za uchaguzi na kuitumbukiza nchi katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika huduma za jamii,” ameonya Jaji Kaijage.
Mhe. Kaijage amesema kuwa hamasa katika siasa za Tanzania imeongezeka sana na kwamba kumekua na ongezeko la hali ya kutokuaminiana haswa katika mchakato wa uchaguzi na kwamba endapo wasimamizi hawatafanya kazi yao kwa ufasaha wataitumbukiza nchi kwenye matatizo makubwa.
“Mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mna uwezo wa kufanya kazi hii, kitu cha muhimu ni kujiamini na kujitambua. Pia kuhakikisha mnayajua vyema maeneo yenu mnayofanyia kazi, kuhakikisha mnawatumia vizuri wasaidizi mlio nao kwa matokeo bora,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...