BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na ufanisi.
Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika linafikia malengo yake muhimu.
Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.
Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo kulia akiwa na Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale wakisikiliza kwa umakini hoja za wafanyakazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...