Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati), Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Kulia), Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor.

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa Tarafa, Mhe Mtaturu alisema kuwa bado uzalishaji wa mazao ni mdogo katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuwa na ardhi nzuri.

Aliwataka wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia wakulima ili kuiwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza umasikini kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula. 
 Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Mhe Mtaturu alisema Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi sambamba na kuhuisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu za umwagiliaji ili wananchi waweze kuzalisha chakula cha kutosha mwaka mzima.


Alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo tayari serikali imetoa tani 20 za mbegu za Pamba katika Wilaya ya Ikungi ambazo zitagawanywa kwa wakulima ili msimu wa kilimo unapoanza tayari ukata wa kucheleweshwa kwa mbegu hizo uwe umetekelezwa.
 Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...