Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.
Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.
Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia. “Mmejifunza mambo mengi,naomba muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...