Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya ISame Mkoa wa Kilimanjaro, Rosemary Sinyamule ameongoza mazoezi ya wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya utamaduni waliojiwekea watumishi na wakazi wa eneo hilo kila ifikapo mwisho wa wiki.
Dc Sinyamule amesesma kuwa mazoezi yamekuwa ni utamaduni hivyo wananchi hao upata fursa ya kujumuika na viongozi wao katika siku ambazo sio za kazi na kuweza kupata nafasi ya kuzungumza mambo ya kawaida yanayohusu maisha yao ya kila siku katika mfumo wa kawaida .
" leo wananchi wamepata fursa muhimu ya kusikiliza maelekezo ya afya kutoka na umuhimu wa mazoezi kutoka Kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Same . Dr. Andrew ambaye aliwataka wakazi wa eneo hilo kutunza afya kwa kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki hili kuweza kujiepusha na magonjwa yasiyokuwa ya lazima" amesema Dc Sinyamule.
DC Sinyamule ameongeza kuwa katika kuadhimisha wiki ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayat Mwl Julius Nyerere ni kila mmoja kuona namna anavyomuenzi kwani alikuwa Mazalendo na alipigania Uhuru akiwa katika umri mdogo hivyo kuwasisitiza Vijana kufanya yale yote yaliyofanywa na Mwalimu katika harakati zake.
DC Sinyamule alimaliza kwa kuwashukuru wananchi wa Same Kwa kuendelea kujitokeza Kwa wingi. Pia aliwakumbusha kila mmoja kujipangia ratiba ya mazoezi kila siku. na si kungoja siku moja Kwa mwezi.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja na Wanachi waliojitokeza katika Mazoezi Wilaya ya Same.Wakazi wa Wilaya ya Same wakiwa katika Mazoezi ya Pamoja yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Rosemary Sinyamule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...