MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeelezwa kuwa, upelelezi dhidi ya kesi ya
kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Face book
kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia,
inayomkabili Mkazi wa Chato Geita, Obadia Kiko bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini amesema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14 mwaka huu.
Katika
kesi hiyo, inadaiwa Agosti 3, mwaka huu huko Chato Geita mshtakiwa
obadia anadaiwa kusambaza maneno kuwa " Taarifa kutoka kikao cha
mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa
wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya
sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni
hivi ni vituko mwizi anakusaidia sheria haahaa haha."
Inadaiwa
aliendelea kusambaza maneno kuwa "Mazungumzo bado yanaendelea lakini
wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo
vyote vya mikataba kiukweli tumuombe mungu maana Serikali ikitaka
kuvunja mkataba na Acacia gharama kubwa zitatuusu."
"Lakini
pia kuendeleza uvyama utatugharimu saana, baada ya mh. Rais Magufuli
angewashirikisha Mawakili wasomi waliokwishaiva wakili Lissu, wakili
Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo ya umuhimu kama haya yeye kaleta
uchama sasa itatugharimu .// Dicteta Magufuli mist go" . Maneno hayo
yanadaiwa kusambazwa na mshtakiwa huyo kupitia mtandao huo wa kijamii wa
Facebook.
Ilidaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kupotosha umma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...