Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za filamu za
Watanzania nchini unakomeshwa mara moja kwa kuwasaka wahusika na
kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema ambapo moja ya changamoto kubwa aliyotajiwa na wamiliki hao ni suala la uharamia wa kazi za sanaa jambo ambalo linawakwamisha wamiliki hao kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakivujisha filamu mpya kwa kuziuza kiholela mitaani na wengine wakihuisha filamu hizo katika mitandao ya kijamii jambo linalosabibisha hasara kubwa kwa wasanii na wamiliki wa majumba ya sinema.
Mhe. Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu hao wanaojihusisha na uharamia wa kazi za filamu za Watanzania huku akiapa kuwashughulikia popote walipo watu hao ili kuhakikisha kuwa Wasanii wananufaika na kazi zao na pia Wamiliki wa Majengo ya Sinema wananufaika pia kwa kuonyesha kazi za wasanii hao kwa utaratibu ambao hautomuumiza msanii mwenye kazi yake.
“Najua baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Sinema mnapata hasara, na hata baadhi ya Wasanii pia, suala hili linanikera sana na kamwe haikubaliki hata kidogo, tutahakikisha kwamba watu wa namna hii wanatoweka katika tasnia yetu, tutawasaka popote walipo na kuwapeleka kwenye vyombo vya Sheria kwani Serikali hii sio ye mchezo na watu wa namna hii”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, yeye kama Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo atahakikisha kwamba hamasa ya kutosha inatolewa kwa Watanzania ili wawe na utamaduni wa kuangalia sinema zinazotengenezwa nchini katika Majumba ya Sinema yaliyopo nchini.

(kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza
(katikati) wakiwa katika moja ya Jumba la Kuonyeshea Sinema lililopo
Jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na
kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11
Oktoba, 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara
hiyo, Bibi Leah Kihimbi.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana
Shonza (kushoto) wakiangalia moja ya kifaa kikubwa kitumikacho
kuonyeshea sinema maarufu kama Projekta wakati walipokutana na Wamiliki
wa Majumba hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na
uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza
(katikati) wakiwa wameongozana na baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya
Kuonyeshea Sinema wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na
kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11
Oktoba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...