Jonas Kamaleki- MAELEZO

Serikali yawataka watanzania kurejesha nchi katika misingi iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuwa na viongozi waadilifu,wazalendo na wenye uchungu na nchi yao.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 18 ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ole Nasha amesema kuwa kumekuwa na ombwe kubwa la kuporomoka kwa maadili, kushamiri kwa rushwa, ufisadi, kukosekana kwa uzalendo na uwajibikaji, kuwepo kwa wafanyakazi hewa na biashara ya madawa ya kulevya.

Ameongeza kuwa wengi waliokuwa wakiharibu nchi hii ni watanzania wenyewe kwa ajili ya tamaa na ubinafsi wao. Nimefarijika sana kusikia kuwa Chuo kimeanza kurejesha hadhi yake iliyokuwepo hapo awali kilipoasisiwa kwa kuanzisha program maalum ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora,”alisema Ole Nasha.

Akizungumzia Mada Kuu ya Kongamano ambayo ni Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri amesema kuwa ni ukweli usiopingika katika uchumi wa maendeleo ya viwanda, Uzalendo, Utaifa, Uadilifu na Uongozi Bora vinapaswa kuzingatiwa. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa viwanda si maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...