Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo pamoja na kusaidia changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii katika karne hii ya 21 hapa nchini.
Dk. Shein aliyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha mika 72 tangu ulipoanzishwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN), hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Mjini Zanzibar ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Umoja huo pamoja na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Mashirika yake ya Maendeleo hapa nchini umeweza kutoa ushirikiano wake mkubwa katika kupambana na umasikini, maradhi, majanga na kusaidia sekta mbali mbali za maendeleo.
Alisema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na taasisi zake umekuwa ukishirikiana vyema na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa mchango wake mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa mipango mbali mbali ya maendeleo katika sekta zote za kiuchumi na kijamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNAIDS katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Leopold Zekeng,wakati alipowasili katika Hoteli ya Serena Zanzibar katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake (katikati) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNAIDS katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Leopold Zekeng,wakati alipowasili katika Hoteli ya Serena Zanzibar jana katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake (katikati) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez.
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na wageni mbali m,bali na waalikwa wakiwa katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika jana katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez wakati akitoa hutuba yake katika sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez (kulia) wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar. Picha na IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...