HAKIMU mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomasi Simba amekwama kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo.
Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo lakini Hakimu Simba amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo na ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu (2017).
Mapema Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.
Wema anashtakiwa pamoja na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...