NI MIEZI MITATU TANGU
ULIPOTANGULIA MBELE ZA HAKI MPENDWAWETU MZEE GALLUS CHOGIMEMBE
NYAKUNGA HAPO TAREHE 12 JULY 2017 KIHESA IRINGA.
HATUTASAHAU UPENDO,
UCHESHI, NA BUSARA ZAKO DAIMA, KIUKWELI PENGO LAKO HALIWEZI KUZIBIKA KAMWE.
UNAKUMBUKWA SANA NA MKE
WAKO MPENDWA YASINTA KIBIKI, WATOTO WAKO, WAKWE NA WAKAMWANA WAKO, WAJUKUU,
VITUKUU, KAKA, DADA NA SHEMEJI ZAKO, NDUGU, JAMAA, MAJIRANI NA MARAFIKI ZAKO.
TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA
ZAIDI, PUMZIKA KWA AMANI.
MKESHA WA KUMALIZA MSIBA
NI TAREHE 13/10/2017, MISA TAREHE 14/10/2017
SAA 12.30 ASUBUHI KANISA LA KIHESA IKIFUATIWA NA KUSIMIKA MSALABA
KIJIJINI NDULI.
TUNAWASHUKURU WOTE KWA
KUTUFARIJI KIPINDI HIKI KIGUMU, MUNGU AWABARIKI.
TUNAWAKARIBISHA KUUNGANA
NASI KATIKA KUHITIMISHA MSIBA HUO NYUMBANI KWAKE KIHESA IRINGA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...