Na Felix Mwagara (MOHA)

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Magereza kumchukulia hatua kali Mkandarasi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete wilayani Kilombero endapo atabainika alifanya makosa kwa kuutelekeza mradi huo.

Mradi huo ambao ungesaidia kuendeleza kilimo cha mpunga na mahindi kwa zaidi ya ekari 1000, unathamani ya zaidi ya Bilioni 2.5 ambapo ulianza kujengwa mwaka 2013 mara bada ya Serikali kumpa Mkandarasi huyo wa Kampuni ya Tanzania Building Works ya Dar es Salaam, zaidi ya Bilioni 1 ili kuufanikisha mradi huo katika hatua ya awali. 

Akizungumza mara baada ya kuukagua mradi huo uliopo Idete mkoani Morogoro, Masauni alisema Serikali ya Awamu ya Tano haitakubali uzembe huo kwa fedha za Serikali kuchezewa huku mradi huo haujakamilika.

Masauni alilitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha Mkandarasi huyo ambaye fedha alizopewa haziendani na ukubwa wa kazi alizozifanya, achunguzwe haraka iwezekanavyo na endapo ikibainika amefanya makosa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

“Fedha ni nyingi alizopewa, zaidi ya bilioni moja za Serikali zimetolewa, na ukiangalia ukubwa wa kazi aliyoifanya haiendani na thamani ya fedha hizo, hivyo hatuwezi kuvumilia na kuona fedha za Serikali zikichezewa, nahitaji huyu mkandarasi achunguzwe na ikithibitika amefanya makosa hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Masauni na kuongeza;

“Fedha zilizotumika ni nyingi halafu mkandarasi huyo eti anaondoka kwasababu ambayo inayojulikana akisingizia kuwa ukosefu wa fedha, Serikali haiwezi ikachezewa, tendo la kuchelewa kwa mradi huu ameitia hasara kubwa Serikali.” 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...