Fainesy Matiholo akishangilia ushindi wake wa kitita cha Milioni 65 akiwa baba na Mama yake Tabora Mjini.
Fainesy
Matiholo, mkazi wa Tabora Mjini ambaye amekuwa akicheza Tatu Mzuka huku
akiwaa kuwa itatokea siku aibuke msndini basi, siku hiyo ikawa ni
Jumapili iliyopita ambapo akaibuka kuwa mshindi wa 12 wa droo kubwa ya
Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.
Bi.
Matiholo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi na Mkuu wa Wilaya ya
Tabora Mheshimiwa Queen Mlozi ambaye alitoa zawadi hiyo akimuwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri. Makabidhiano hayo
yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.
“Nimekuwa
nikicheza Tatu Mzuka kila juma lakini lengo langu kubwa lilikuwa kupata
ushindi wa kila saa. Sikutarajia kabisa kuwa nitaibuka mshindi wa droo
kubwa ya Tatu Mzuka,” anasema.
Katika
hafla hiyo ya kukabidhi zawadi, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Bi. Mlozi alizungumza kuwa; “tumefurahi sana kuona kuwa juma hili
mshindi wa Tatu Mzuka katika katika Mkoa wetu. Ushindi huu umetusaidia
kuamini kuwa mchezo huu unatoa fursa sawa kwa watu wote. Naamini sasa
wananchi wa Tabora watahamasika zaidi kushiriki katika mchezo huu.”
Katika
ushindi huu wa Bi. Matiholo pia rafiki zake watatu ambao hushiriki
kucheza Tatu Mzuka nao wamefanikiwa kujishindia kiasi cha Shilingi
milioni 1 kila mmoja kupitia kipengele cha Tatu Mzuka “cheza na washkaji
na washikaji promosheni.” Walioshinda kipengele hiki ni Jacqueline
Samuel, Sande Kabaye na Lilian Tegete.
“Tatu
Mzuka imebadili maisha yangu,” Bi. Matiholo anasema na kuongeza kuwa;
“naweza sasa kuanza kupanga namna ya kuishi maisha bora zaidi, nitaweza
kumpatia mwanangu elimu bora zaidi na pia kuboresha biashara yangu,“
alieleza.
Hata
wewe unaweza kuwa mshindi ajaye wa Tatu Mzuka na safari hii mshindi
anatarajiwa kupata kitita kinachofikia milioni 110. Hadi sasa kumekuwepo
na washindi zaidi ya milioni 1.7 waliojishindia zawadi mbalimbali
kutoka Tatu Mzuka. Pia kuna zaidi ya shilingi milioni 500 zinazosubiriwa
kushindaniwa kadri siku zinavyoenda. Unaweza kuwa mshindi lakini jambno
la kufanya ni kushiriki mchezo huu mara nyingi zaidi uwezavyo.
Fainesy Matiholo mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.
Mheshimiwa
Queen Mlozi Mkuu wa Wilaya wa Tabora akitoa zawadi kwa Fainesy Matiholo
akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey
Mwanri.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...