Balozi
wa Danube Home, Zarina Hassan akizungumza baada ya uzinduzi wa duka la
Danube Home na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye duka
la lao kwa ajili ya kujipatia bidhaa zenye ubora na thamani nafuu.
Waziri
wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage akipata maelekezo wakati alipotembelea maeneo mbalimbali
ndani ya duka la Danube HomeMlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi
wa wateja waliojitokeza katika ufunguzi wa duka la Danube Home wakiwa
wanaangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye duka hilo jana Jijini
Dar es salaam.
WAZIRI
wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka kampuni ya Danube
Home na GSM kuendelea kuwekeza nchini kwani wanaposema uchumi wa viwanja
ni pamoja na biashara za samani kama wanazojishughulisha nazo.
Mwijage ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la Danube Home uliofanyika jana Mlimani City pamoja na kutambulishwa kwa balozi wa Danube nchini Tanzania Zarina Hassan.
Akizungumza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka hilo, Mwijage amesema kuwa anatarajia kuona Danube wanatumia malighafi zinazopatikana nchini kwa ajili ya kutengenezea samani mbalimbali za ndani ikiwemo masofa, vitanda na zinginezo kwani zinapatikana kwa urahisi.
"Natarajia kuona mnatumia samani zinazopatikana nchini, pia nimesikia hapa mkisema katika maandalizi ya kufungua duka hili mmewatumia zaidi watanzania na hicho ni kitu kizuri na ninaamini mtaendelea kuwaamini watanzania",amesema Mwijage.
Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan amewashukuru watanzania kwa ukarimu mkubwa waliokuwa nao na zaidi Tanzania ni eneo salama kwa ajili ya kufanya biashara kwani kwa kushirikiana na kampuni ya GSM wameweza kufungua duka la tatu.
Kampuni ya GSM na Danube Home zimeweza kutoa ajira zaidi ya 1000 kwa nchini huku aslimia 99 wakiwa ni watanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...