Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo
la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji
mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.
Katika
maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba
yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia
wananchi kwa ajili ya matumizi.
Naibu
Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo
inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa
changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.
“Nitakaa
na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili
kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya
wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.

Fundi wa DAWASCO akiendelea
na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO
Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la
Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua
moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...