
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa hana mpango wa kufuta mbio za mwenge wa uhuru kutokana na madai ya baadhi ya watu wanaosema kwamba hauna faida.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Zanzibar alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
“Mwenge wa Uhuru hatutaufuta kwa sababu unachochea maendeleo, katika kipindi cha uongozi wangu na Dkt. Shein Mwenge utaendelea kukimbizwa nchini kote,” alisisitiza Rais Magufuli.Alisema kuwa baadhi ya watu wanaodai kwamba mwenge huo unaleta hasara kutokana na gharama zinazotumika, wazingatie kuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni ndogo ukilinganisha na faida kubwa inayopatikana kupitia miradi inayotekelezwa kutokana na hamasa ya mbio za mwenge kwenye maeneo mbalimbali kote nchini.
Aidha alibainisha kuwa mwenge wa uhuru ni moja ya tunu za nchi ya Tanzania na alama ya uhuru na utaifa wetu hivyo kuufuta ni sawa na kufuta alama kubwa inayotambulisha nchi yetu.“Mwenge huu unatuunganisha watanzania na kuimarisha muungano wetu na yeyote atakayejaribu kuharibu amani au kuvuruga muungano tutapambana naye,” alisema Rais Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...