Na TIGANYA VINCENT-RS-TABORA

SERIKALI mkoani Tabora imesitisha likizo kwa muda kwa Maafisa Ugani na Watumishi wote wanaowatakiwa kuwasaidia wakulima ili waweze kulima kilimo kinachozingatia utalaamu kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao mengi na kwa tija.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo na Seketarieti ya Mkoa huo.

Alisema kuwa wakati msimu wa mvua unakaribia kuanza sio vema watumishi wa kada hiyo wakaanza likizo kwani wanapaswa kutumia kipindi hicho kuwafanya kazi ya kuwasaidia na kuwaelimisha wakulima ili wafanye vizuri katika shughuli zao na kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kupitia mavuno mazuri watakayopata.

Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa likizo ni haki ya mtumishi inabidi wazingatie kuwa likizo zao haziathiri wakulima katika kipindi hiki muhimu kwa ajili ya kilimo.Alisema kuwa baada ya shughuli za kilimo kukaa vizuri Maafisa hao wanaweza kuendelea na likizo zao ikiwa watakuwa wamehakikisha kuwa kwenda kwao likizo hakutakuwa na athari kwa wakulima.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Maafisa Ugani wote kuondoka maofisini na kwenda kwa wakulima katika kipindi hiki ili kuhakikisha kila mkulima anazingatia kanuni bora za kilimo kulingana na mazao anayolima.Alisema kuwa lengo ni kutaka Mkoa wa Tabora uwe mfano wa kuigwa katika ulimaji wa kilimo cha kisasa na chenye tija.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...