Na Pamela Mollel-Arusha

Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwakutafuta maji.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.

Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat  watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya kifugaji.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii  ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora.
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)
 Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii.
  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...