Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amempa mwezi mmoja Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba, kujenga vyoo bora katika Mnada uliopo Kijiji cha Malendi, kata ya Mgongo Wilayani humo.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mnada huo ambapo wananchi wamelalamika kukosa huduma za vyoo na maji kwa kipindi kirefu huku halmashauri ikikusanya ushuru bila kuwaboreshea miundombinu ya mnada huo.

“Mkurugenzi nakupa mwezi mmoja hapa kuwe na vyoo bora vikiwa na matundu sita kwa ajili ya wananchi hawa pamoja na huduma za maji, kipindi cha mvua kinaanza, lazma muwajali wananchi hawa kwakuwa kipindupindu kinaweza kulipuka hapa”, ameeleza Dkt Nchimbi.

Ameongeza kuwa kwakuwa hakuna vyoo wananchi watajisaidia maeneo ya jirani na mnada na mvua zikianza zitatiririsha uchafu huo katika eneo la mnada na makazi ya wanakijiji cha Malendi na hivyo kusababisha mlipuko wamagonjwa hasa Kipindupindu.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliokuwa wamepanga foleni kulipa ushuru katika mnada wa Malendi Wilayani Iramba.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akikagua mnada wa Malendi Wilayani Iramba ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anajenga vyoo na kufikisha huduma za maji ndani ya mwezi mmoja.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Malendi na maeneo ya jirani waliokuwa katika mnada huo wakinyoosha mikono kumsalimia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowatembelea mnadani hapo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...