Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (kulia), akimkabidhi kipeperushi cha taasisi hiyo, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili wagonjwa wa moyo, kusaidia kufanyiwa upasuaji, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 10, 2017 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (wa tatu kulia), mfano wa hundi ya sh. milioni 4 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wawili wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa TPC, ulipotembelea taasisi hiyo katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani, Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto, Dkt. Godwin Sharau na wa kwanza ni Meneja Mkuu Usimamizi Biashara wa TPC, Hassan Mwang'ombe.
Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (wa tano kulia), akiwapatia maelezo baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika ulipotembelea moja ya wodi za wagonjwa wa moyo kwenye taasisi hiyo leo jijini. Wa nne kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akiwa amembeba mtoto Delphina, ambaye ni mmoja wa watoto waliopatiwa msaada wa sh. milioni 2 kila mmoja na TPC kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea kwenye wodi za wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili Dar es Salaam leo katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...