Mmoja wa viongozi wa Chama cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) Rehema Athuman ( kulia) akimjulia hali Mzee Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga, Kata ya Kisaki, wilaya ya Morogoro ambaye alikatwa sehemu ya mkono wake wa kushoto ambaye juzi aliletwa kutoka kituo cha Afya Duthumi na kulazwa hosipitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kuendelea na matibabu zaidi. ( Picha na John Nditi).

Na John Nditi, Morogoro

CHAMA cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) kimewaomba  viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali kujikita kutoa elimu kwa wananchi  ili waweze kubadili mitazamo na kuacha kuwadhuru  wenye ualbino  kutokana na imani za kishirikina  na wambue  nao ni binadamu sawa na  walivyo wengine.

Mwenyekiti wa TAS Taifa, Nemes Temba  alisema hayo hivi karibuni ( Okt 5)  mjini hapa baada ya kumjulia hali mwenzao Nassoro Msingili (75) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyarutanga,  Kata ya Kisaki , wilayani Morogoro  mwaka huu baada ya kufanyiwa ukatili  Oktoba 3, mwaka huu na baadhi ya  watu kumkata mkono  wa kushoto na kutokomea nao.

Temba alisema,   kitendo cha Mzee Msingili kukatwa mkono kimewaumiza  wao kama  watu wenye ualbino na taifa kwa ujumla na kukemea  vikali  kitendo hicho kwa kuwa kufuatia tayari ameongezewa  ulemavu mwingine zaidi ya ualbino aliokuwa nao.

Alisema kuwa  kwa wastani asilimia kubwa  ya  suala la mauaji, kukatwa viungo na kunyanyaswa kwa watu wenye ualbino ni ya kishirikina   ambao unapaswa kukemewa na kupingwa vita na kila Mtanzania.

Hivyo alimwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk  John  Pombe Magufuli  kulitolea tamko la kukemea vikali vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino nchini ili waweze kuishi kwa  amani sawa na watanzania wengine.

waandishi wa Habari mjini Morogoro  juu ya wao kukemea vikali kitendo cha ukatili alichofanyiwa albino mwenzao Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga Kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro vijijini Oktoba 3 mwaka huu.

“ Natoa  wito kwa viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali  washiriki kutoa elimu kwa wananchi  ili wabadili  mitazamo na kuacha kuwadhuru albino kwa imani za kishirikina  na badala yake atambue  kuwa  albino nao ni binadamu kama walivyo watu wengine” alisema Temba.

Hata hivyo aliiomba Serikali kufanya jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine kuweza kupata takwimu sahihi za ualbino ili kuweza  kuwalinda  na kupatia huduma muhimu .

Msingili (75) alikatwa mkono wa kushoto mnamo Oktoba 3 ,mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Nyarutanga , kata ya Kisaki,  wilayani Morogoro baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana  wakati akiwa amelala nyumbani ,na kulazwa  katika Kituo cha afya Duthumi  ambapo juzi alihamishiwa  Hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Morogoro  kwa  ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Akizungumza na gazeti hili juzi , akiwa wodi ya majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Msingili alisema kuwa wakati akivamiwa usiku alikuwa peke yake kwa kuwa ndugu zake walikuwa wamehamishia makazi ya muda shambani  kuvuna nafaka.

Alisema kuwa akiwa amelala usiku watu wasiofahamika walimvamia nyumbani kwake na walimpiga na kitu butu kama rungu kichawani na alipojihami kwa kuinua mgomo wake wa kushoto juu ghafla akikatwa na panga na  watu hao kutokomea na sehemu ya mkono wake wa kushoto.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonce Rwengasira,alisema kufuatia tukio hilo Polisi inawashirikia watu wawili kwa tuhuma hizo ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili upelelezi bado unendelea kufanyika na watafikishwa mahakamani wakati wowote ule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...