Na.Vero Ignatus,Dodoma
Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC)
inaeendesha mafunzo ya siku (5) ya waandishi habari za mazingira
(27)mkoani Dodoma, kwa waandishi kutoka mikoa yote nchini ikiwa ni awamu
wa kwanza
Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko amesema kuwa lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwapata waandishi waliobobea katika kuandika habari za mazingira katika maeneo yao.
"Unapowapata wabobezi hawa ni rahisi kwa wadau wa habari kutoka mikoani kufanya kazi na waandishi amabao wapo madhubuti kwenye maeneo yao,wapo waandishi wengi makanjanja hawajui wanachokifanya"alisema Victor.
Mafunzo mengine yanayoendeshwa sambamba na haya ni pamoja na mkoani Pwani yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Jinsia ,mkoani Morogoro yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Vijijini na mkoani Dodoma mafunzo ya uandishi wa habari za Mazingira
"tunataka
tuwapate machampion watakao simamia habari za mazingira peke
yayake,Jinsia pamoja na waandishi wa habari za vijijini tu"alisema
Amewaasa
waandishi wa habari ambao hawajajiunga katika vilabu vya waandishi
habari vilivyopo kila mkoa wajiunge kwani zinawasaidia kuwakutanisha
pamoja watanufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na UTPC ,ambapo
amesema mafunzo kama haya hayawezi kutolewa kwa mwandishi ambaye siyo
mwanchama .
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale
amesema kuwa lazima mwandishi awe na malengo,waandike habari zinazoleta
mabadiliko na zinazogusa hisia za jamii kwa ujumla.''Mwandishi kama
unaandika kila kitu muda wako unakaribia kwisha"alisema Mfugale.
Amesema
kuwa UTPC itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa habari
chini ufadhili wa Ubalozi wa Sweeden hapa nchini kwa muda wa miaka (5)
ambapo huu ni mwaka wa( 2) hadi 2020 wataendelea kubadilisha mafunzo
hayo kadri ya uhitaji wa waandishi .
Muwezeshaji wa mafunzo Deodatus Mfugale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Centurion Nala Hotel Dodoma
Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko akizungumza na waandishi katika Mafunzo hayo mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...