Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Masuala ya Ukuzaji wa Amani , Haki za Binadamu na Misingi ya haki za binadamu (AREPEB) limeandaa mafunzo ya kuelimisha jamii juu ya amani na utatuzi wa migogoro pamoja na Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora yatakayofanyika Oktoba 7 na 8 mwaka huu Kibaha, mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti na Msemaji Mkuu wa Shirika hilo Angela Masha amesema kuwa mafunzo yatayofanyika yatajenga wananchi juu ya kufanya utatuzi wa migogoro hata baina ya yao.

Amesema katika uelimishaji huo wamezindua namba ya kukusanya maoni juu ya ukuzaji wa amani nchini na pamoja na taarifa za masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kutuma ujumbe bure kupitia namba 0800712121 au 0757 333 773 na ujumbe wa sauti kwa namba 0758333773.

Mwenyekiti huyo amesema mfumo wa mawasiliano ni huru kwa wananchi pasipo na ubaguzi wowote hivyo wananchi hao watumie katika uchangiaji wa maoni katika ukuzaji wa amani, Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala bora.

Angela amesema amani iliyopo nchini ni muhimu kwa ujenzi wa nchi ya viwanda , ukuzaji wa uchumi, maendeleo ya mtu mmoja mmoja pamoja na uzalishaji mali na Demokrasia.
 Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Yohana Mcharo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, katikati ni Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Bi. Angella Mushi na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.
Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi.Angella Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...