VIOGOZI
wa vyama vya walemavu barani Afrika wakutana jijini Dar es Salaam
kwaajili ya kujadili maswala mbalimbali ya walemavu pamoja na kuwa na
sera ya pamoja ya walemavu barani Afrika.
Maswala na sera wanazozijadili ni pamoja na maswala ya
kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ambapo yatawapa fursa walemavu kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Shirikiso la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA),
Ummy Ndeliananga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa bara la
Afrika unaoendelea kufanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.
Tunatakiwa
kuwa na sauti ya pamoja watu wenye ulemavu barani Afrika ambapo
tutakuwa na hatua tofautitofauti pia ametoa wito kwa serikali kujenga
miundombinu ambayo inafikika kwa walemavu wote katika bara la Afrika.


Watafsiri
wa Lugha za Alama kutoka Kenya na Uganda wakitafsiri mazungumzo
yaliyokuwa yakiendelea ya kuunda sera ya pamoja ya walemavu wa bara
Afrika.
Mtafsiri
wa lugha za Alama kulia azingumza na watu wenye ulemavua ambao ni
viziwi ili kwenda pamoja katika mkutano utakao fanyika kwa siku mbili
ambapo walemavu watajadiliana masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu,
kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi
za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza.
Mkurugenzi
mtendaji wa Muungano wa walemavu Afrika kutoka nchini Afrika Kusini
(Africa Disability alliance), Dagnachew Wakene akizungumza wa viongozi
mbalimbali wavyama vya walemavu barani Afrika wakizungumza maswala
mbalimbali ya walemavu na kuunda sera ya pamoja kwa bara la Afrika.
Mratibu
wa Mkutano wa viongozi wa watu wenye ulemavu, Oktaviani Simba
akizungumza katika mkutano unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam
leo.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu barani afrika wakiwa katika mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...