Na Robert Hokororo, Kishapu
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
limekutana kwa ajili ya kuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya
kata zake mbalimbali.
Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba,
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo aliipongeza Kishapu kwa
kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG). Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani waendelee
kushikamana na kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kuleta maendeleo katika
halmashauri ya wilaya hiyo.
Alisema ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao
sambamba na kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususan cha mazao
yanayostahimili ukame.
“Waheshimiwa tuwahudumie wananchi katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa
Serikali inapigania katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe
kulima,” alisema.
Aliongeza kuwa katika kikao hicho Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya
maendeleo na wapi wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye
kusonga mbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga
akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za
kata.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akifungua kikao
cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa halmashauri.
Madiwani wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...