Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akipokea Hundi yenye thamani ya Sh. Millioni 20 kutoka kwa Mkurugenzi Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Zanzibar Novemba 9, 2017. CRDB imekabidhi hundi hizo wa Rais Dkt. Shein ikiwa ni ahadi iliyoahidiwa na Benki hiyo kwa ajili ya mchango kwa Mfuko wa Rais kwa maendeleo ya uwezeshaji, sambamba na kupokea Milioni tano kwa ajili ya Ujenzi katika Skuli ya chekechea Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akimkabidhi zawadi ya karafuu Mkurugenzi Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Zanzibar Novemba 9, 2017. CRDB imekabidhi hundi zenye thamani ya Sh. Millioni 20 kwa Rais Dkt. Shein ikiwa ni ahadi ya Benki hiyo kwa ajili ya mchango kwa Mfuko wa Rais kwa maendeleo ya uwezeshaji, sambamba na kupokea Milioni tano kwa ajili ya Ujenzi katika Skuli ya chekechea Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wa nne kulia) na ujumbe wake, katika hafla fupi ya kukabidhi hundi zenye thamani wa milioni 20 kwa ajili ya mchango kwa Mfuko wa Rais kwa maendeleo ya uwezeshaji, sambamba na kupokea Milioni tano kwa ajili ya Ujenzi katika Skuli ya chekechea Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba, iliyofanyika Ikulu, Zanzibar Novemba 9, 2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mkurugenzi Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, Ikulu Zanzibar Novemba 9, 2017. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...