Ikiwa ni msimu mpya wa ufunguzi wa vyuo mbalimbali nchini, Benki ya CRDB
imewapa ahueni kubwa wanafunzi wa elimu ya juu katika vyuo mbalimbali
nchini kwa kusogeza huduma za kibenki katika maeneo yanayotumika
kufanya usajili wa wanafunzi. Kupitia matawi yake yanayotembea na wakala
wa benki (FahariHuduma), Benki ya CRDB imeweza kupeleka huduma za
kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na
wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine
za chuo.
Ukiondoa huduma za kuweka na kutoa fedha, zoezi la ufunguzi wa akaunti
maalum ya wanafunzi ya Scholar limekua likifanyika ili kuwawezesha
wanafunzi hususani wale wanaopokea mikopo ya elimu ya juu kuweza
kutunza fedha zao kwa usalama. Katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
ambacho kina jumla ya vitivo saba ndani yake, Benki ya CRDB imeweza
kusogeza huduma za kifedha katika vitivo vyote saba pamoja na kuwa na tawi
na mashine za kutolea fedha katika vitivo vyote.
Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa
kwanza katika Chuo cha Dodoma Ikupa Mwambene amesema, “tunaishukuru
sana Benki ya CRDB kwa kuweza kutusogezea huduma hadi katika vitivo
vyetu kwani imeweza kuturahisishia zoezi kufanya usajili na kuokoa muda
mwingi”. Nae Afisa Uhusiano wa chuo hiko Bi. Beatrice Baltazar amesema
kuwa uwepo wa huduma za benki zinatozolewa na Benki ya CRDB umeweza
kuwapa unafuu mkubwa wanafunzi kwa kuwa ilikua ikiwalazimu kwenda nje
ya chuo kufata huduma za kibenki kasha kurudi chuoni ili kufanya usajili
jambo lililokua linachukua muda mwingi sana.
Baadhi ya wanafunzi wapya wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipatiwa huduma za kuweka na kutoa fedha kutoka Benki ya CRDB kupitia matawi yake yanayotembea na wakala wa benki (FahariHuduma), ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
Wakala wa FahariHuduma wa Benki ya CRDB akichukua taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wakatika walipowasogezea huduma za kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma wakiendelea kupatiwa huduma kutoka kwa Maafisa wa Benki ya CRDB wa tawi lake linalotembea na wakala wa benki (FahariHuduma),
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...