Taasisi
ya Dr Mtuyabaliwe imekabidhi Chumba cha maktaba, ilichokikarabati na
kukisheheni vitabu, kwa shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa
Temeke, ambayo tangu kuanzishwa kwake miaka 30 iliyopita haikuwahi kuwa
na maktaba.
Akikabidhi
Maktaba hiyo Mkurugenzi na Muasisi wa Taasisi ya Dr Ntuyabakiwe
Jacquiline Mengi amesema Taasisi hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2015 kumuenzi
marehemu baba yake aliyekuwa mpenzi mkubwa wa kusoma vitabu, inahimiza
usomaji wa vitabu kwa wanafunzi,ikiwa ni kuunga mkono jitihada za
serikali za kutoa elimu bora nchini:
Katika
salaamu zao za shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Bakari
Makele, Mwalimu Mkuu Esther Matowo na Dada mkuu Veronika Mruma
wameshukuru kwa msaada huo na kuahidi kuitunza na kuitumia ipasavyo.
Wakati
wa hafla hiyo Mwakilishi Taasisi ya Sema-Tanzania Itanisa Mbise
alikabidhi kwa Dada Mkuu wa shule Veronica Mruma nakala 100 za jarida
linalochapishwa na Taasisi hiyo kwa matumizi ya maktaba hiyo.
Makabidhiano
ya Makataba hiyo kwa shule ya Msingi Muungano yamefanyika wakati ambao
Wizara ya elimu imeingiza somo la Maktaba katika mtaala wa elimu baada
ya kuona umuhimu wake katika kufanikisha utoaji wa elimu katika shule za
msingi.
Dr
Ntuyabaliwe Foundation ni taasisi pekee binafsi nchini inayojihusisha
na utoaji wa misaada ya vitabu vya maktaba kwa shule za msingi nchini,
na hadi sasa imekwishatoa misaada kama huo kwa shule mbili za msingi za
jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu
vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muungano
waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akikata utepe kuashiria
uzikizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi pamoja na walimu na
wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo katika
shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke
Mwalimu
Mkuu ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo akisoma risala kwa mgeni
rasmiwakati wa zoezi la uzinduzi wa maktaba shuleni hapo leo. wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi na
wapili kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke, Bakari Makele.

Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...