Na David John

MWENYEKITI wa Shirikisho la Waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdallahaman Lutenga Amesema chini ya uongozi wake atahakikisha hakuna fisadi wala mchwa yeyote atakaengia kwenye shirikisho hilo.

Amesema kuwa wanachama wa shirikisho hilo lazima watambue kuwa shirikisho hilo ni mahala patakatifu na viongozi wanaokwenda kuongoza shirikisho lazima wawe waadilifu na wenye uchungu na si vinginevyo.

Lutenga ametoa kauli hii mapema leo katika mahojiano maalum ambapo alikuwa anajibu hoja mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa shirikisho hilo.

Amesema kuwa anasikia malalamiko na hoja ambazo zinatolewa na baadhi ya waganga hususani wakihoji uhalali wa yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti ambapo amesema yeye yupo kwa mujibu wa Katiba yao na Kama kuna watu hawataki basi wanaweza kwenda Mahakamani. 

Mwenyekiti huyo taifa amesema kuwa yeye ataendelea kuwa mwenyekiti hadi uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakapofanyika mwishoni mwa 2018 nakudai kuwa wajumbe wa halmashauri kuu kwa mujibu wa katiba yao kwa Kauli moja waliwaongezea muda ili kukamilisha baadhi ya mambo.
Mwenyekiti wa shirikisho la waganga wa tiba asili Tanzania Abdallahaman Lutenga akifafanua jambo kuhusu tuhuma mbalinbali ambazo zinatolewa na baadhi ya wanachama wa shirikisho hilo.picha na David John.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...