Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa kata za Kigamboni, Vijibweni, Tungi zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika  kufuatia kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mgalu aliyasema hayo  tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati  itahakikisha  vituo vingine vya kuboresha  hali ya umeme ndani ya jiji la  Dar es Salaam  vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa  tatizo la  kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza.

Aidha, alilitaka  Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kukamilisha vituo  vingine  vilivyobaki vya Kurasini, Gongo la Mboto na Mbagala mapema ili wakazi wa jiji la Dar es Salaam waweze kuondokana na  tatizo la ukosefu wa umeme.Katika hatua nyingine, Mgalu aliwataka wandarasi waliopewa kazi ya kujenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) kukamilisha miradi mapema na kuongeza kuwa  Serikali haitamvumilia mkandarasi atakayezembea ukamilishwaji  wa mradi wake.
 Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam, Sylvester Sikare (kulia) akielezea maendeleo ya ukamilishaji wa kituo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) mara alipofanya ziara katika kituo hicho tarehe 27 Novemba, 2017.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Richard Swai (kushoto mbele) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) katika ziara hiyo.
 Moja ya transfoma zilizopo katika kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni  kilichopo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.


 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...