Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza na
wataalam, wanahabari na viongozi wa Wizara hiyo kutoka katika sekta ya Uvuvi,
baada ya kuonyeshwa zana zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya
kupambana na uvuvi haramu, katika kanda ya Dar es Salaam.
baadhi ya zana zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa
katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika kanda ya Dar
es Salaam.
Akiwa katika zoezi la kupongeza kikosi maalum kilichoanza oparesheni ya
kupambana na uvuvi haramau katika bahari ya hindi leo, zoezi lililokwenda
sambamba na kuonyeshwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu
vilivyokamatwa katika zoezi hilo lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa
mifugo na Uvuvi Mhe. Luahaga Mpana amezitaka halmashauri ambazo shughuli
za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.
Mpina ambaye ameshangazwa na kitendo cha Halmashauri hizo kukusanya fedha
za ushuru zitokanazo na shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa kuingia katika
zoezia la kupambana na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za kufanya
doria.
Aidha, Mpina Amewataka viongozi wakuu wa Wizara yake, Katibu Mkuu Dkt.
Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi wa maeneleo ya Uvuvi Bw. Magese Bulayi
kutembea na barua rasmi katika ziara zao za kikazi kwenye halmashauri husika
zilizokuwa tayari kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la
kupambana na uvuvi haramu.
“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi na katibu Mkuu,nawaagiza mtembee na
barua zilizotayari kusimamisha au kufukuza kazi watumishi wazembe katika
halmashauri, barua hizo zibaki wazi katika sehemu ya kujaza majina yao tuu, na
ndani ya mwaka mmoja nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “ Alisisitiza
Mpina.
Awali akieleza madhara ya matumizi ya kitoweo cha samaki waliyovuliwa kwa njia
ya vilipuzi na mabomu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba alisema
kuwa samaki wanaovuliwa kwa njia hiyo huleta madhara makubwa kwa walaji
ikiwa ni mapoja na magonjwa ya tumbo na Saratani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...