Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro akikagua askari wa Mkoani Pwani alipofanya ziara mkoani humo kukagua utendaji kazi wa askari. IGP amewasisitiza askari wa Mkoa wa Pwani kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa huo.
 Askari wa kikosi maalum cha Mkoani Pwani cha kupambana na majambazi kwenye majengo makubwa wakifanya zoezi baada ya IGP kuwasili mkoani humo kukagua utendaji kazi wa askari.
 Askari wa kikosi maalum cha Mkoani Pwani cha kupambana na majambazi kwenye majengo makubwa wakifanya zoezi baada ya IGP kuwasili mkoani humo kukagua utendaji kazi wa askari.
Inspekta Jeneralibwa Polisi, IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. IGP yupo mkoani Pwani kwa ziara ya kufanya ukaguzi kuona utendaji kazi wa askari ili kuona changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi. 
Picha na Hassan Mndeme wa Jeshi la Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...