Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Novemba 28/2017 imemuhuku mfanyabiashara Gairo Mtozoma (43), kutumikia kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia kukutwa na silaha pamoja na risasi.

Mshtakiwa Gairo ambaye pia ni mkazi wa Magomeni Kagera amehukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mwambapa amesema, upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka hayo na kwamba baada ya kusikiliza ushahidi huo  mahakama ilimuona mshitakiwa kuwa na kesi ya kujibu na kujitetea mwenyewe.

Amesema kuwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mashitaka ya kwanza  ya kupatikana na silaha, mshitakiwa huyo atatakiwa  kutumikia kifungo cha miaka mitano jela na katika mashitaka ya pili atatumikia kifungo cha miaka mitano.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa wengine.

Katika kesi ya msingi, inadaiwa Agosti 11,2016 maeneo ya Magomeni Kagera wilayani Kinondoni, Mshtakiwa Gairo alikutwa na bastola moja aina ya Browing yenye kumbukumbu  namba 90002 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR-A222683 bila kuwa na leseni.

Pia inadaiwa Agosti 11,2016 maeneo ya Magomeni Kagera wilayani Kinondoni alikutwa na risasi sita bila kuwa na leseni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...