Meza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
Bw. Lunda Asmani akiwakaribisha wadau wote na kufungua jukwaa la afya.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba yake kwenye kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt, Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kuthamini kazi kubwa inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi yao.
Balozi wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana na miundo mbinu kuwa duni na sababu kubwa inachangiwa na wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije ukaongoza Dunia.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru Diaspora kwa mchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani zake na kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...