LEO TAREHE 30.11.2017 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI (PICHANI), AMEKANUSHA TAARIFA ILIYOPO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI LA TAREHE 30/11/2017, TOLEO NAMBA 6334, UKURASA WA TATU, INAYOSEMA KUWA AMETHIBITISHA JUU YA KUWEPO HEWA YA SUMU NDANI YA UKUMBI WA CITY MALL AMBAPO KULIKUWA KUKIFANYIKA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA VIJANA WA CCM (UVCCM) MKOA WA MWANZA.

AIDHA KAMANDA MSANGI ANASEMA, UKWELI NI KUWA ALIPIGIWA SIMU NA MWANDISHI WA GAZETI HILO TAREHE 29/11/2017 MAJIRA YA SAA 15:00 MCHANA ALIYETAKA KUTHIBITISHIWA TAARIFA YA KUWEPO HEWA YA SUMU NDANI YA UKUMBI WA CITY MALL AMBAPO KULIKUWA KUKIFANYIKA MKUTANO TAJWA HAPO JUU.
KAMANDA ALIMJIBU KUWA HANA TAARIFA NA HAWEZI KUTHIBITISHA KWANI HAJAPATA TAARIFA YEYOTE KUHUSIANA NA YALIYOTOKEA KATIKA MKUTANO HUO, NA YEYE YUPO KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA OFISI YA MKUU WA MKOA.
PIA KAMANDA HAKUFIKA ENEO TAJWA KAMA TAARIFA HIYO INAVYOSEMA, HIVYO INAONEKANA MWANDISHI WA TAARIFA HIYO ALIAMUA KUANDIKA MANENO HAYO KWA MANUFAA YAKE BINAFSI HIVYO JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAOMBA GAZETI HUSIKA KUREKEBISHA. PIA ANAOMBA WAELEWE KUWA MATUKIO YA AINA KAMA HIYO YANAHITAJI YAWE NA MAJIBU YA KITAALAMU TOKA KWA WANASAYANSI PINDI YANAPOTOKEA.
AIDHA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINANAEDELE KUOMBA USHIRIKIANO TOKA KWA WAANDISHI WA HABARI KWA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA ILI KUWEZA KUENDELEA KUDUMISHA USALAMA NA ULINZI KATIKA MKOA WETU. PIA JESHI LINAWAOMBA WAANDISHI WA HABARI KUFANYA KAZI KWA KUFUATA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI, UWELEDI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI ILI KUEPUSHA HABARI ZA AINA KAMA HII AMBAZO ZINALETA PICHA MBAYA KWA JESHI NA MKANGANYIKO KWA JAMII.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
Kamanda Msangi yuko sahihi anaposema kuwa masuala kama haya yanahitaji majibu ya kitaalamu kutoka kwa wanasayansi. Katika kuunga mkono hoja yake, napenda tu nifafanue kuwa tuelewane kuwa sayansi ni dhana ambayo tunapaswa kuielewa kwa mapana kuliko tulivyozoea.
ReplyDeleteKisayansi, kwa namna jamii inavyoelewa dhana hiyo, suala la kuwepo au kutokuwepo gesi ya sumu linaweza kutolewa majibu na wakemia. Hao ni baadhi ya wanasayansi wanaohitajika hapo. Lakini, kemia peke yake haiwezi kutoa majibu juu ya mambo yanayosababisha, kudumisha, kueneza, au kuaminika kwa uvumi. Uvumi unaweza kushamiri hata bila kuwepo kwa uhalisia wa jambo kwa kigezo cha kemia. Hata wanakemia wakathibitisha kuwa hapakuwa na sumu katika hewa, uvumi unaweza kubaki vile vile, na unaweza kushamiri.
Hapo ndipo zinapohitajika taaluma zingine, kama hiyo ya saikolojia ya jamii ("social psychology") au taaluma kama yangu ya "Folklore." Katika "Folklore" tunatafiti mambo menage, ikiwemo uvumi, yaani "rumour." Kuna vitabu na makala nyingi kuhusu "rumour," kuelezea chimbuko lake, na mantiki yake. Kuna watafiti maarufu kama Jan Harold Brunvand, ambayo wanatambulika ulimwenguni kwa utafiti wao na yale wanayotufundisha.
Huu uvumi uliozuka Mwanza umefungamana na siasa. Ni kiashiria cha hali ya kisiasa nchini. Kwa mujibu wa taaluma ya saikolojia ya siasa, au saikolojia ya jamii, au "Folklore," hatuwezi kusema tu kwamba kwa kuwa hapakuwa na sumu katika hewa ndani ya ukumbi ule, basi suala limeisha. Itakuwa ni kujidanganya. Panahitajika utafiti na uchambuzi wa dhati.