NA TIGANYA VINCENT

KUCHELEWA kupelekwa fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi ili waweze kukamilisha Mradi wao wa Ujenzi wa jengo la Mashine ya Usindikaji wa Mafuta katika Kijiji cha Kombe umesababisha Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kupewa wiki mbili kuhakikisha fedha hizo zinafika haraka la sivyo atakuwa amejiundoa kazini mwenyewe.

Msimamo huo umetolewa jana wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Mashine ya kukamulia mafuata ya alizeti ambao umekwama kumalizika kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya Halmashauri kuchelewa kupeleka fedha ambazo ilitakiwa itoe.

Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wamejituma kujenga jengo kwa ajili ya kuweka mashine ya kusindika mafuta ya alizeti lakini  Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua hadi hivi sasa hajitoa milioni 4 zilizotakiwa kuunga mkono nguvu za wananchi hao.

 Aidha Mwanri aliongeza kuwa pia kiasi kingine ni zile milioni 17 zilizotolewa na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Miombo kwa ajili shughuli mbalimbali kama vile ufugaji kuku, kilimo cha uyoga, ufugaji nyuki zimekwama kupelekwa kwa walengwa kwa sababu ya Ofisi ya Uhasibu ya Halmashauri hiyo kuchelewesha wakati Wilaya nyingine zimeshapeleka kwa walengwa na kuanza kufanyakazi. 

Alisema kuwa hawezi kumvumilia mtumishi wa sampuni hiyo ambaye ameshindwa wa kutumia fedha miradi kwa wakati ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika kuwainua kiuchumi na kuwaletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa sababu ya urasimu usio na maana kwani kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...