Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amesema kuwa madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani, hatawavumilia kuendelea kumiliki leseni walizozipata.

Muslimu aliyasema hayo wakati alipokutana na vyama vya madereva jijini Dar es Salaam, amesema madereva lazima wafuate sheria za usalama bila kufanya hivyo leseni zao zitafutwa.Amesema udereva ni kazi zilivyo kazi zingine hivyo lazima kazi hiyo iheshimike kwa kufuata sheria za usalama barabarani barabarani kutokana na asilimia 80 ya uchumi inabebwa na madereva hao.

Kamanda Muslim amesema ameomba majina ya madereva kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambao wanachezea vidhibiti mwendo ili aweze kufunga leseni za madereva wanaofanya mchezo huo.

Nae Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano amesema kuwa kazi ya madereva kupandisha nauli sio kazi yao kwani wanaotakiwa ni wamiliki kupeleka maombi Sumatra juu ya gharama za uendeshaji,Kahatano amesema suala la madereva kulalamikia mikataba ya ajira haliko kwao na badala yake kazi hiyo itafanywa na idara ya ajira ambao ndio wanaweza kujua juu mikataba ya maderva jinsi itavyokuwa.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim akizungumza katika mkutano wa vyama vya madereva juu kufuata sheria za usalama barabarani, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano akizungumza na madereva jinsi Sumatra inavyofanya kazi katika kuhakikisha huduma za usafiri zinatolewa bila mwananchi kupata kikwazo, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya madereva waliofika katika Mkutano na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...