MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Nyong’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisifu juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto za afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili wananchi kupata huduma bora 

Proffesa Maji Marefu aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa tiba kwa Halmashauri ya Korogwe Vijijini vilivyotolewa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia Bohari ya Madawa MSD wamewapatia vitanda vya kulalia wagonjwa,magodoro na mashuka vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni 17.

Vifaa tiba hiyo kwa upande wa vitanda vya wagonjwa vitasambazwa kwa baadhi ya vituo vya Afya na Zahanati zilizopo wilayani humo ambavyo ni Magoma, Mombo, Bungu,Mazinde,Manka,Hale,Mashewa,Vugiri na MakumbaKwa upande wa vitanda vya kuzalishia vitapelekwa kwenye zahanati za Mandera,Kwemazandu,Lwengera,Mkomazi na Makumba ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali.

“Niwaambieni tu serikali yenu chini ya Rais Dkt John Magufuli imejipanga vema kuhakikisha inatatua kwa vitendo changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ya huduma za afya na ndio maana leo hii tunakabidhi vifaa hivi kwa lengo la kuboresha huduma hizo “Alisema.

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Korogwe Vijijini

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mombo mashuka kwa niaba ya Vituo vya Afya vyengine kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Korogwe Vijijini kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dkt Frank Chiduo na kushoto ni Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Korogwe Vijijini
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani Alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia akiteta jambo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo kuhusu umuhimu wa vifaa hivyo kutunza ili kuweza kuwahudumia wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...