Na Clarence Nanyaro – NEC 

ARUSHA.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya Siasa na wadau mbalimbali wa Uchaguzi kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani utakaofanyika kesho (Jumapili) Novemba 22, 2017 unafanyika kwa amani na Utulivu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga Kura.

Akisoma risala kwa umma leo Jijini Arusha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa Wapiga Kura wapatao 333,309 wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 43 za Tanzania Bara na kuongeza kuwa uchaguzi huo utafanyika katika Vituo 884 vya Uchaguzi ambako ndipo Wapiga kura walijiandikishia kupiga kura katika Uchgauzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015.

Amesema kuwa tofauti na Chaguzi zilizopita,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuzingatia masharti ya sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa kifungu cha 62 imewaruhusu wapiga kura ambao ama kadi zao za kupigia kura zimepotea au kuchakaa au kufutika kutumia vitambulisho mbadala kwenda katika vituo walivyojiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi huu.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa masharti ya Mpiga Kura kuruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala yatazingatia sharti la kwamba majina ya mpiga kura lazima yafanane kwa herufi na majina yaliyoko katika kitambulisho mbadala ambayo yako katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...