Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae na Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni katika chumba cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya.
1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya asubuhi hii ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika leo katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. 

Picha na Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...