Mkongwe katika mitindo nchini Tanzania na Marekani maarufu kama Mama wa mitindo Bi. Asya Idarous Khamsin anatarajiwa kuonyesha mitindo yake mbalimbali ya ubunifu wa mavazi katika sherehe ya maalum ya Watanzania itakayofanyika tarehe 9 Desemba,2017 huko Oakland California Nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Mama wa Mitindo, Bi. Asya Idarous Khamsin ameweka wazi kuwa, onyesho hilo litakuwa la aina yake kwani watu watakaojitokeza watashuhudia mitindo mipya kabisa ya mavazi ambauyo itaonyesha kwenye jukwaa maalum siku hiyo sambamba na Chakula maalum cha kuchangia watu wenye tatizo la ugonjwa wa Kansa nchini Tanzania.
“9 Desemba,2017 tumewaandalia onyesho maalum la mavazi. Watu wajitokeze kwa wingi kushuhudia mavazi ya ubunifu. Pia kutakuwa na ‘fundraising dinner’ ya kukusanya fedha kwa ajili ya (partnering to tackle cancer to Tanzania) ambayo inafanyika kila mwaka.
Sherehe hizo ni pamoja na kusherehekea Shamla shamla za Uhuru wa (Tanganyika) ambayo sasa ni Tanzania” Alieleza Asya Idarous Khamsin.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...