Wakati Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), ikianza leo Novemba 02, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tayari limezilipa timu zote sita zinazoanza kuchuana hatua ya awali.

Mchezo kati ya Kisarawe United ya Pwani na Silabu ya Mtwara umeahirishwa hadi hapo baadaye utakapotangazwa tena kwa sababu ya majeruhi ya wachezaji. Baadhi ya wachezaji wa Silabu – mabingwa wa Mkoa wa Mtwara wameumia kutokana na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mchinga mkoani Lindi wakiwa safarini kwenda Pwani.

Mechi zinazochezwa ni kati ya Buseresere ya Geita itayocheza na Isako ya Songwe; ilihali Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga katika mechi hizo za awali kuwania taji la ASFC.

Baada ya mechi hizo, itakuja Raundi ya Kwanza ya ASFC ambayo itachezwa kati ya Novemba 7, 8 au 9 ambako TFF imepanga kesho Novemba 2, mwaka huu kutuma fedha zote za maandalizi ya timu husika ili kusiwe na kisingizio chochote cha kujiandaa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred ameagiza Idara ya Fedha na Utawala ya TFF kulipa fedha hizo haraka, lakini kwa masharti ya taratibu za malipo kwamba lazima yapitie benki, badala ya akaunti ya mwakilishi ye yote au kiongozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...